Tuesday, 9 May 2017

                                            kukatishwa kwa misaada nchini kenya 
Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) ambao hutumiwa na Marekani kutoa misaada kwa nchi za nje, limesitisha ufadhili wake kwa miradi ya afya nchini Kenya.Taarifa kutoka kwa shirika hilo imesema hatua ya kusitisha ufadhili kwa miradi yote ya Wizara ya Afya ya Kenya imetokana na hatua ya Kenya kutotimiza masharti ambayo hayajaelezwa
Akizungumza Maafisa wa USAID wameagizwa kutojishughulisha na shughuli zozote za kibiashara na taasisi za serikali ya Kenya pamoja na mashirika mengine yenye uhusiano na serikali Hatua hiyo ya Marekani inatarajiwa kuathiri miradi mbalimbali ya serikali ikiwemo mipango ya kukabiliana na malaria, kifua kikuu na Ukimwi pamoja na miradi ya uzazi wa mpango, huduma za afya kwa wajawazito na watoto.
Kwa miezi kadha sasa, wizara ya afya nchini Kenya imekubwa na tuhuma za ulaji rushwa.
Sekta ya afya Kenya pia ilitatizwa na mgomo wa taifa madaktari namo mwaka jana Desemba madaktari wakenye waligoma kwa siku 100, pia mkaguzi mkuu wa hesabu nchini humo alisema jumla ya dola milioni 50 hazikutumika katika wizara ya afya kama ilivyo tarajiwa. 


Hata hivyo maafisa katika wizara ya afya pamoja na baadhi ya viongozi nchini humo walidaiwa kuhusika katika ufujaji wa pesa hizo, lakini Wizara ya nchi hiyo ilijitetea kwa kukanusha habari hizo.Hatua ya USAID inatarajiwa kuathiri sana miradi ya serikali pamoja na miradi ya mashirika mengine ya afya ambayo hutumiwa na USAID kutoa huduma maeneo mbalimbali Kenya.http://www.bbc.com/swahili/habari-3985

No comments:

Namna ya kupika Vitumbua Vitumbua ni aina ya vitafunwa vya chai ambavyo hutengenezwa kwa kutumia unga wa mchele. Kiasili vitumbua ni ch...