UREMBO



                                   urembo wa kucha na aina ya rangi  na utunzaji wake


unashauriwa kwamba kabla ya kuchukuwa uamuzi wa kwenda kupaka rangi pamoja na kununua vifaa husika ambayo unataka kuvitumia unapaswa kufahamu aina ya kucha ili uweze kununua vifaa vinavyoendana na kucha zako kwa lengo la kuzilinda badala ya kuvamia na kuziharibu.Kwa kawaida kucha za mikononi na miguuni zinakabiliwa na mazingira magumu kutokana na majukumu ya kazi za kila siku hali inayochangia kuziweka katika mazingira magumu kiafya. 
Mbali na kucha kukosa afya, pia kuharibu shepu yake ya awali kutokana na shughuli za kila siku katika maisha ya binadamu yeyote, hivyo ni vyema kuzikinga kucha zako na maradhi kwa kuzifanyia usafi kila siku au mara kadhaa kwa wiki ili kuzilinda zaidi. 

Ili kuweza kugundua aina ya kucha zako katika kuzipangilia wakati wa kuzifanyia usafi, unapaswa kuwa makini wakati unachagua rangi ya kupaka, kuangalia muonekano wa kucha zako zilivyo ili uweze kupangalia rangi ziweze kuwa na mvuto zaidi. kama kwenye picha ya hapo juu
rangi za kucha za mikono unaweza ukachagua moja ili kulingana na ngozi yako ili upendeze na utokelezeee mwanamke urembo
 

No comments:

Namna ya kupika Vitumbua Vitumbua ni aina ya vitafunwa vya chai ambavyo hutengenezwa kwa kutumia unga wa mchele. Kiasili vitumbua ni ch...