mahitaji
- Ndizi mbichi 15
- Nyama ya ng'ombe ( kilo moja)
- Viazi mviringo 6
- Kitunguu swaumu
- Tangawizi
- Kitunguu maji
- Nyanya 1 kubwa
- Mafuta (vegetable oil)
- Chumvi
- Limao
- Pilipili
Matayarisho
1.Chemsha nyama
2. limao
endelea
kitunguu swaum, tangawizi chumvi na maji kiasi mpaka nyama iive, Hakikisha unaiacha na supu kiasi kwa ajili ya kuwekea kwenye ndizi.Kisha katakata nyanya na vitunguu na uweke pembeni .Menya ndizi na viazi kisha zichemshe pamoja na vitunguu, nyanya, maji kidogo, mafuta na uhakikishe haziivi kabisa. Baada ya hapo tia nyama na supu yake, pilipili mzima na chumvi na uache uchemke mpaka ndizi na viazi viive.Na baada ya hapo mchemsho wako utakuwa tayari kwa kuliwa
No comments:
Post a Comment