Thursday, 11 May 2017

                                           
                                                 KUMBUKUMBU YA BOB MARLEY


Alianza muziki miaka ya 1960 akiwa na kundi lake la kina Wailing Wailers, ambalo alilianzisha akiwa na marafiki wawili, Peter Tosh na Bunny Wailer. Mwaka wa 1962, Bob Marley na kina Wailing Wailers wakafanikiwa kurekodi nyimbo zao mbili za kwanza zilizoitwa “Judge Not” na “One Cup of Coffee”.
Bob alimuoa Bi. Rita Anderson mwaka 1966 na akajiunga na kundi akiwa kama mwitikiaji. Kwa pamoja wamefanikiwa kupata watoto watano. Mmoja kati ya hao ni Ziggy Marley, ambaye pia ni mwimbaji wa reggae maarufu.
Mwaka wa 1974, pamoja na kundi la Wailers kutengana, Bob Marley aliendelea kuita bendi yake jina la Bob Marley and the Wailers na kujiunga upya na wanachama wapya huku wakindelea kupiga muziki kama kawaida. Mwaka wa 1975, Bob Marley akatoa wimbo wake wa kwanza ambao ulimpa umaarufu duniani kote, ulijulikana kama “No Woman No Cry”.
Baadhi ya nyimbo zake kali ni pamoja na “I Shot the Sheriff”, “Could You Be Loved”, “Stir It Up”, “Jamming”, “Redemption Song”, “One Love” na, “Three Little Birds”.
Bob Marley alifariki katika hospitali ya Cedars of Lebanon Hospital huko mjini Miami, Florida, kwa tatizo la melanoma (kansa ya ngozi).

Tuesday, 9 May 2017

                                            kukatishwa kwa misaada nchini kenya 
Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) ambao hutumiwa na Marekani kutoa misaada kwa nchi za nje, limesitisha ufadhili wake kwa miradi ya afya nchini Kenya.Taarifa kutoka kwa shirika hilo imesema hatua ya kusitisha ufadhili kwa miradi yote ya Wizara ya Afya ya Kenya imetokana na hatua ya Kenya kutotimiza masharti ambayo hayajaelezwa
Akizungumza Maafisa wa USAID wameagizwa kutojishughulisha na shughuli zozote za kibiashara na taasisi za serikali ya Kenya pamoja na mashirika mengine yenye uhusiano na serikali Hatua hiyo ya Marekani inatarajiwa kuathiri miradi mbalimbali ya serikali ikiwemo mipango ya kukabiliana na malaria, kifua kikuu na Ukimwi pamoja na miradi ya uzazi wa mpango, huduma za afya kwa wajawazito na watoto.
Kwa miezi kadha sasa, wizara ya afya nchini Kenya imekubwa na tuhuma za ulaji rushwa.
Sekta ya afya Kenya pia ilitatizwa na mgomo wa taifa madaktari namo mwaka jana Desemba madaktari wakenye waligoma kwa siku 100, pia mkaguzi mkuu wa hesabu nchini humo alisema jumla ya dola milioni 50 hazikutumika katika wizara ya afya kama ilivyo tarajiwa. 


Hata hivyo maafisa katika wizara ya afya pamoja na baadhi ya viongozi nchini humo walidaiwa kuhusika katika ufujaji wa pesa hizo, lakini Wizara ya nchi hiyo ilijitetea kwa kukanusha habari hizo.Hatua ya USAID inatarajiwa kuathiri sana miradi ya serikali pamoja na miradi ya mashirika mengine ya afya ambayo hutumiwa na USAID kutoa huduma maeneo mbalimbali Kenya.http://www.bbc.com/swahili/habari-3985

Msanii kutoka kundi la Jambo Squad la Jijini Arusha, Chalii ya Jambo a.k.a Mtoto wa Bibi, mwishoni mwa juma lililopita aliamua kufunga pingu za maisha na namekusongezea baadhi ya picha kutoka kwenye harusi hiyo
Akiandika katika ukurasa wake na kusema Asante Mungu kwa kunipa hili Tunda .. Nashkuru siku ya Jana nimefunda ndoa Salama . #AboutYesterday hongera mtoto wa bibi😊😊😊💙💗💗

Namna ya kupika Vitumbua Vitumbua ni aina ya vitafunwa vya chai ambavyo hutengenezwa kwa kutumia unga wa mchele. Kiasili vitumbua ni ch...